Highlights

Vijana 35 Marsabit wakamilisha tathmini ya TVET mashinani.

Na JB Nateleng

Shirika la Caritas Marsabit kwa ushirikiano na wakaguzi kutoka Nyeri National Polytechnic limeendesha tathmini ya mwisho kwa vijana 35 waliokuwa wakipata mafunzo chini ya mpango wa wezesha vijana TVET Mashinani.

Tathmini hiyo iliyofanyika katika maeneo ya Korr na Moyale imewapa washiriki hao nafasi ya kuonesha ujuzi waliopata katika kozi mbalimbali. Vijana waliokuwa Korr walitathminiwa katika ukarabati na ujuzi wa kutengeza pikipiki, huku wale wa Moyale wakitathminiwa kuhusu ujuzi wa oka Mikate na Keki.

Hatua hiyo inatarajiwa kuwawezesha vijana hao kupata vyeti vya kitaaluma na kuwapa uwezo wa kujiajiri, kupata ajira na kuanzisha shughuli za kiuchumi zitakazoboresha maisha yao.

Radio Jangwani 106.3FM is a community radio station situated in Marsabit County broadcasting from Marsabit town. It is the brain child of the bishop of catholic diocese of Marsabit, Rt. Rev. Peter Kihara. It is established with the objective of reaching the people Marsabit diocese and Marsabit County for evangelization, Education, entertaining and disseminating information to the masses.

Post Comment