KUPPET Marsabit yapinga uchaguzi wa viongozi wa wanafunzi shuleni
Na Sabalua Moses
Katibu mkuu wa chama cha kuwatetea walimu wa shule za upili na vyuo vya anuwai KUPPET tawi la Marsabit Sarr Galgalo amesema kuwapa wanafunzi nafasi ya kujichagulia viongozi wao shuleni unadunisha nidhamu kwa asilimia kubwa .
Akizungumza na shajara ya redio jangwani kwa njia ya simu Galgallo amesema kuwa mara nyingi wanafunzi hutaka kuchagua viongozi wanaotetea haki zao jambo linaloweza kuathiri nidhamu na usimamizi wa shule.
Vile vile, Galgallo amesema kuwa walimu kuchagua wanafunzi ni bora zaidi licha ya kutaka kuendeleza demokrasia shuleni.
Hata hivyo ,Galgallo amewahimiza wazazi kushughulikia hali ya nidhamu ya wana wao ili kupunguza utovu wa nidhamu shuleni huku akitaka serikali kuwachukulia hatua kali wanafunzi wanaoteketeza shule.
Kwa upande wake Mohammed Hassan ambaye ni mwaraharakati kaunti ya Marsabit, nafasi ya kupata viongozi wao kutawapa mwelekezo mzuri na kukuza umuhimu wa demokrasia nchini.



Post Comment