Highlights

Ukavu kuendelea kushuhudiwa Marsabit katika kipindi cha siku saba- Idara ya hali ya anga yadokeza

Na Caroline Waforo

Idara ya Hali ya Hewa Kaunti ya Marsabit imetoa utabiri wa hali ya hewa kwenye ripoti yake ya kila wiki inaonyesha kuwa sehemu kubwa ya kaunti inatarajiwa kuwa kavu huku mvua zikitarajiwa kunyesha katika maeneo machache.

Kulingana na utabiri huo wa kuanzia tarehe 9 hadi 15 mwezi huu wa Juni , maeneo yatakayoshuhudia ukavu ni pamoja Marsabit mjini, Karare, North Horr, Dukana, Maikona, Turbi, Kargi, Laisamis, Loglogo, Korr, Ngurunit, Loiyangalani pamoja na maeneo mengi ya kaunti ndogo ya Moyale.

Mvua chache zitashuhudiwa katika baadhi ya maeneo machache yaliyo karibu na Mlima Marsabit, Sagante Jaldesa, Maikona, Sololo pamoja na maeneo machache yanayopakana na Ethiopia

Ukungu nyakati za asubuhi na jioni unatarajiwa kushuhudiwa katika maeneo yaliyo karibu na mlima Marsabit

Katika ukanda wa Loiyangalani na Ziwa Turkana, hali ya joto kali na upepo mkali inatarajiwa kutawala. Upepo huo unaweza kusababisha mawimbi makubwa ziwani, vumbi na kupungua kwa uwezo wa kuona.

Radio Jangwani 106.3FM is a community radio station situated in Marsabit County broadcasting from Marsabit town. It is the brain child of the bishop of catholic diocese of Marsabit, Rt. Rev. Peter Kihara. It is established with the objective of reaching the people Marsabit diocese and Marsabit County for evangelization, Education, entertaining and disseminating information to the masses.

2 comments

comments user
Valerie

What’s Happening i am new to this, I stumbled upon this I’ve discovered It positively useful and it has
aided me out loads. I’m hoping to give a contribution & help other users like its helped me.
Great job.

comments user
Clinton

Wow, that’s what I was looking for, what a material!

present here at this blog, thanks admin of this site.

Post Comment