Ruto aahidi kufufua miradi ya maji na umeme Marsabit

Na JB Nateleng
Serikali ya Kitaifa inatekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo katika Kaunti ya Marsabit yenye thamani ya mabilioni ya fedha inayolenga kufungua uchumi wa eneo hili kupitia uwekezaji katika miundombinu, biashara, maji, nishati na huduma za afya.
Akizungumza kwenye mkutano uliowaleta pamoja viongozi baadhi ya wananchi kutoka kaunti ya Marsabit kwenye Ikulu ya Nairobi hii Leo Ruto amesema kuwa mradi wa Bwawa la Badassa ni miongoni mwa miradi ambayo serikali itaharakisha kukamilisha ili kuongeza upatikanaji wa maji safi kwa wakazi wa kaunti hiyo.
Pia ameongeza kuwa serikali ya kitaifa itashirikiana na serikali ya kaunti kutafuta suluhu ya kudumu kwa changamoto ya maji.
Ruto amesema serikali inaendelea kusambaza nishati kupitia miradi ya mini-grid katika maeneo mbalimbali ya Marsabit kwa lengo la kuhakikisha wakazi wengi zaidi wanapata huduma ya umeme kutoka kwenye gridi ya kitaifa.
Ruto amefichua kuwa serikali imetenga shilingi milioni 390 kwa ajili ya kupeleka umeme katika eneo la Loiyangalani, huku mradi huo ukitarajiwa kukamilika kufikia Desemba mwaka huu.
Kadhalika Ruto ametangaza mpango wa kuimarisha usafiri na biashara kati ya Kaunti za Marsabit na Turkana kupitia huduma ya meli katika Ziwa Turkana, akisema mradi huo unalenga kurahisisha usafirishaji wa watu na bidhaa kati ya kaunti hizo mbili.



Post Comment