Sport Bulletins

Draw Ya Kombe La FA Awamu Ya Robo Fainali Yatolewa

Taji La FA
Picha;Hisani

By Waihenya Isaac,

Draw Ya Kombe la FA awamu ya Robo Fainali yatolewa huku mechi hizo zikiratibiwa kupigwa tarehe 20 na 21 mwezi machi mwaka huu.

Bingwa wa Kombe hilo mwaka wa 2019 Manchester City watasafiri hadi ugani Goodson Park kumenyana na Everton katika kampeni ya kusaka taji lao la 6 la FA.

Vijana wa Brendan Rodgers Leicester City watatoana kijasho na bingwa mara 12 wa taji hilo   Manchester United Katika uga wao wa nyumbani wa King Power Stadium.

Kocha Mpya wa klabu ya Chelsea Thomas Tuchel atasaka nafasi ya kunyakua taji lake la kwanza kama mkufunzi wa klabu hiyo watakapoikarisha Sheffield United ugani Stamford Bridge.

Aidha Bournemouth watawakaribisha Southampton FC waliombandua bingwa mtetezi Arsenali Katika raundi ya 6 ya michuano hiyo.

Subscribe to eNewsletter