Highlights

Shirika la SND lataja ushirikiano kuwa nguzo ya maendeleo Marsabit.

Na Nyabande Orwa

Ushirikiano kati ya serikali ya kaunti, mashirika ya maendeleo na wadau wengine umetajwa kuwa nguzo muhimu ya kukuza umoja, mshikamano na maendeleo ya kiuchumi kwa wakazi wa kaunti ya Marsabit.

Akizungumza wakati wa maadhimisho ya siku ya kimataifa ya ushirika yaliyofanyika katika uwanja wa wa michezo wa Saku, mkurugenzi wa programu ya Range katika shirika lisilo la kiserikali la SND, Mohamed Wario, amesema kuwa kuwawezesha wananchi kiuchumi ndiyo njia bora ya kupunguza umasikini na kuhakikisha rasilimali zilizopo katika kaunti hiyo zinawanufaisha wakazi wake.

WhatsApp-Image-2026-07-04-at-18.47.03-1024x768 Shirika la SND lataja ushirikiano kuwa nguzo ya maendeleo Marsabit.
Baadhi ya bidhaa ya vyama vya ushirika katika hafla ya kuadhimisha siku ya ushirika Marsabit

Wario amesema kupitia programu ya RANGE, wakazi wa Marsabit wamewezeshwa kutumia rasilimali zilizopo katika kaunti hiyo kujiongezea kipato na kuboresha maisha yao.

Aidha, ametoa wito kwa wananchi kuendeleza amani na kuimarisha ushirikiano kupitia vyama vya ushirika na mashirika mbalimbali ya kijamii ili kuchochea maendeleo endelevu.

Katika hafla hiyo, mashirika ya kijamii kutoka kaunti nne zinazofadhiliwa na shirika la SND yalishiriki kwa kuonyesha bidhaa na huduma mbalimbali zinazotokana na shughuli zao za kiuchumi na maendeleo.

Post Comment