Highlights

NCCK Marsabit, yatoa wito wa Amani msimu huu wa pasaka.

Na JB Nateleng

Mwenyekiti wa baraza la kitaifa la makanisa humu nchini (NCCK), tawi la Marsabit, mhubiri Saido Diba ametoa wito wa amani wakati huu wa Pasaka.

Akizungumza na waandishi wa habari, Diba amesema wakristo na viongozi wanafaa kukumbatia maridhiano badala ya kulipiza kisasi ili kufurahia maendeleo na kuboresha uchumi wa wananchi.

Aidha, amelaani mashambulizi ya hivi majuzi yaliyotokea mjini Marsabit, akisema hayakubaliki, na kuitaka idara ya usalama kufanya uchunguzi wa kina na kuwachukulia hatua wahusika.

Kauli hiyo imeungwa mkono na mwakilishi wadi wa Marsabit Central, Jack Elisha, ambaye amewahimiza wananchi kushirikiana na vyombo vya usalama ili kuimarisha usalama katika eneo hilo.

Post Comment