Highlights

Mwanaume mmoja ahukumiwa kifungo cha miaka 10 gerezani kwa kosa la unajisi, North Horr

Mahakama ya Marsabit imemhukumu mwanaume mmoja kifungo cha miaka 10 gerezani kwa kosa la kumnajisi msichana wa umri wa miaka 11 katika eneo la Mbarambata eneobunge la North Horr kaunti ya Marsabit.

Mhukumiwa Apola Lokayelo Denge amepatikana na hatia ya kumnajisi mtoto huyo mnamo tarehe 4 mwezi Julai mwaka 2025 ambaye pia amepatikana na kosa la kumshika visivyo msichana huyo.

Hukumu hiyo ilitolewa hapo jana Jumatano na Hakimu Mkuu Mwandamizi wa mahakama ya Marsabit Christine Wekesa.

Mwanaume huyo ana siku 14 kukata rufaa dhidi ya hukumu hiyo.

Radio Jangwani 106.3FM is a community radio station situated in Marsabit County broadcasting from Marsabit town. It is the brain child of the bishop of catholic diocese of Marsabit, Rt. Rev. Peter Kihara. It is established with the objective of reaching the people Marsabit diocese and Marsabit County for evangelization, Education, entertaining and disseminating information to the masses.

Post Comment