Vijana wazidi kutiwa shime kupigania haki zao nchini.
January 21, 2025
Na Isaac Waihenya
Waziri wa fedha Njuguna Ndung’u hii leo anatarajiwa kusoma Bajeti ya 2023/24.
Hii ndiyo bajeti ya kwanza ya utawala wa Rais William Ruto na Waziri Ndung’u anatarajiwa kusoma makadirio ya Ksh.3.6 trilioni.
Kamati ya Fedha ya Bunge la Kitaifa inapendekeza nyongeza ya Ksh.80.7 bilioni, huku jumla ya bajeti ikitarajiwa kufikia Ksh.4.4 trilioni.
Serikali ya Kitaifa imetengewa Ksh.2.2 trilioni, huku Idara ya Mahakama ikitengewa Ksh.22 bilioni.
Bunge (Bunge la Kitaifa na Seneti) kwa wakati huo huo limepewa Ksh.41 bilioni.
Kwa sasa, deni la Kenya limetengewa Ksh.1.6 trilioni na serikali inatarajia kukopa Ksh. bilioni 720.1 zaidi.
Akizungumza na vyombo vya habari waziri Njuguna alisema kwamba serekali inalenga sera zitakazosaidia kupiga jeki uchumi wa nchi kupitia makadirio hayo ya leo.