Vijana wazidi kutiwa shime kupigania haki zao nchini.
January 21, 2025
Na Isaac Waihenya
Rais Wiliam Ruto ameelezea kujitolea kwa serekali ya Kenya Kwanza kuimarisha maisha ya mwananchi wa chini.
Rais Ruto aliyasema hayo katika ukumbi wa KICC jijini Nairobi wakati wa uzinduzi wa mpango wa kuwapa uwezo wahudumu wa bodaboda kote nchini.
Mpango huo pia unawapa wanabodaboda mbinu bora ya kujiimarisha kiuchumi huku wakinufaika na bima ya kitaifa ya bei nafuu.
Aidha Rais Ruto aliwahimiza wanabodaboda kote nchini kujiunga na vyama vya ushirika.
Kadhalika Rais Ruto alikariri hoja ya kuwekwa mikakati ya kupunguza ajili zinazosababishwa na bodaboda huku akitaja kwamba takwimu nchini zinaonyesha kwamba bodaboda ndio wanachangia ajili nyingi kati za zile zinazoripotiwa humu nchini.