Highlights

Mwanaume ashtakiwa kwa tuhuma za kumnajisi msichana wa miaka 15, Marsabit Central

Mwanaume mmoja amekamatwa na kushtakiwa katika mahakama ya Marsabit kwa tuhuma za kumnajisi msichana wa miaka 15 katika kijiji cha Manyatta Ginda kaunti ndogo ya Marsabit Central.

Mshukiwa Molu Jillo anadaiwa kutekeleza kitendo hicho siku ya Jumatano ya tarehe 28 mwezi huu wa Januari na kukamatwa hapo jana Alhamisi.

Mbele ya hakimu mkuu mkaazi wa mahakama ya Marsabit Christine Wekesa, mshukiwa amekana kosa dhidi yake na kuachiliwa kwa bondi ya shilingi 200,000.

Aidha hakimu amemwamuru mshukiwa kuwasilisha pasipoti yake mahakamani hadi kesi hiyo itakapoamuliwa.

Kesi hiyo itatajwa tena tarehe 4 mwezi ujao wa Februari.

Post Comment