Highlights

Mlinzi akamatwa kufuatia uporaji wa duka moja mjini Marsabit

Mlinzi mmoja amekamatwa na kushtakiwa katika mahakama ya Marsabit kuhusiana na kisa ambapo wezi wasiojulikana walivunja duka la kuuza mavazi lililoko mkabala na Madrassa ya Taqwa mjini Marsabit, na kuiba mali yote iliyokuwemo usiku wa kuamkia jana Alhamisi.

Kulingana OCPD wa Marsabit Central Beethoven Gachago, uchunguzi unaendelea ili kuwakamata washukiwa wengine waliohusika na wizi huo.

Gachago amewashauri wafanyabiashara mjini Marsabit kushirikiana na pia kuwekeza katika kamera za CCTV ili kulinda biashara zao.

Aidha, amewahakikishia wananchi wa Marsabit Central kuwa idara ya usalama imeimarisha doria kuwahakikishia usalama wao.

Radio Jangwani 106.3FM is a community radio station situated in Marsabit County broadcasting from Marsabit town. It is the brain child of the bishop of catholic diocese of Marsabit, Rt. Rev. Peter Kihara. It is established with the objective of reaching the people Marsabit diocese and Marsabit County for evangelization, Education, entertaining and disseminating information to the masses.

Post Comment