Highlights

Mwanamke afariki baada ya kushambuliwa na ndovu Marsabit

Na Abdiaziz Yusuf

Mwanamke mmoja mwenye umri wa makamo amefariki dunia baada ya kushambuliwa na kukanyagwa na ndovu katika msitu mbuga la Wanyama katika kaunti ya Marsabit.

Akithibitisha tukio hilo, Kamishna wa kaunti ya Marsabit, Stanley Kamande, amesema mwanamke huyo alikumbana na mauti yake alipokuwa akitafuta kuni mbugani.

Kamande amewataka wakazi, hasa wanaoingia msituni kutafuta kuni, kuwafahamisha maafisa wa huduma ya wanyamapori kenya (KWS) kabla ya kuingia na kutumia njia rasmi ili kupunguza hatari ya kushambuliwa na wanyamapori.

Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hifadhi ya maiti ya hospitali ya rufaa na mafunzo ya Marsabit.

Radio Jangwani 106.3FM is a community radio station situated in Marsabit County broadcasting from Marsabit town. It is the brain child of the bishop of catholic diocese of Marsabit, Rt. Rev. Peter Kihara. It is established with the objective of reaching the people Marsabit diocese and Marsabit County for evangelization, Education, entertaining and disseminating information to the masses.

Post Comment