Washukiwa wanne wafikishwa mahakamani Marsabit kwa makosa ya kupanga njama ya mauaji
Na Mwandishi wetu
Watu wanne wamefikishwa katika Mahakama ya Marsabit hii leo Jumatatu na kushtakiwa kwa makosa matatu.
Mbele ya hakimu mkuu mkazi wa mahakama ya Marsabit, Christine Wekesa, washukiwa hao Ali Yattani, Mohammed Hassan, Abdub Jarso na Barako Athe pamoja na washukiwa wengine ambao hawakufika mahakamani, wameshtakiwa kwa makosa ya kupanga njama ya kumuua, kutishia kumuua na kujaribu kumgonga mlalamishi, Godana Gollo Watta.
Kulingana na stakabadhi za mashtaka, washukiwa hao wanadaiwa kutekeleza makosa hayo kati ya tarehe 28 mwezi Mei 2026 na tarehe 3 Juni 2026 katika eneo la Bale, Lokesheni ya Saru, kaunti ndogo ya Dukana.
Washukiwa hao, hata hivyo, wamekana mashtaka yote dhidi yao. Kesi hiyo inatarajiwa kutajwa tena tarehe 19 Agosti na kusikilizwa tarehe 20 Agosti.



Post Comment