Highlights

Mifugo 251 iliyoibwa Loiyangalani yarejeshwa

Na Caroline Waforo

Maafisa wa usalama wamefanikiwa kurejesha kondoo na mbuzi 251 waliokuwa wameibwa na washukiwa wa wizi wa mifugo katika kaunti ndogo ya Loiyangalani kaunti ya Marsabit.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka Idara ya Polisi (NPS), maafisa walifuatilia mifugo hiyo hadi maeneo ya Lokilipi na Sarima, ambapo kulizuka majibizano ya risasi kati ya washukiwa waliokuwa na silaha na maafisa wa usalama.

Kutokana na makabailiano hayo washukiwa walitelekeza mifugo hiyo kabla ya kutoroka.

Mifugo yote 251 ipo chini ya ulinzi wa polisi ikisubiri kutambuliwa na kukabithiwa wamiliki wake halali.

Idara ya Polisi (NPS) imetoa onyo kali kwa wanaojihusisha na wizi wa mifugo, ikiahidi kuendelea kuwalinda wananchi na mali yao.

Radio Jangwani 106.3FM is a community radio station situated in Marsabit County broadcasting from Marsabit town. It is the brain child of the bishop of catholic diocese of Marsabit, Rt. Rev. Peter Kihara. It is established with the objective of reaching the people Marsabit diocese and Marsabit County for evangelization, Education, entertaining and disseminating information to the masses.

Post Comment