Highlights

Mbunge wa North Horr Wario Adhe aitaka vitengo vipya vya utawala Illeret kuanzishwa kwa haraka.

Na Samuel Kosgei

MBUNGE wa North Horr, Wario Guyo Adhe, ameitaka serikali kuu kuharakisha uanzishaji wa vitengo vipya vya utawala katika Kaunti Ndogo ya Illeret, akisema upungufu wa vitengo hivyo unatatiza utoaji wa huduma, uratibu wa usalama na mwitikio wa dharura.

Akizungumza bungeni, Adhe ameomba taarifa kuhusu kile alichokitaja kuwa uwepo usioridhisha wa Vitengo vya Utawala vya Serikali ya Kitaifa (NGAO) katika kaunti ndogo hiyo yenye eneo kubwa linalopakana na Ethiopia.

Mbunge huyo amesema Illeret ina ukubwa wa zaidi ya kilomita za mraba 4,000 kandokando ya mpaka wa Kenya na Ethiopia, lakini kwa sasa inahudumiwa na chifu mmoja na naibu chifu mmoja pekee. Alisema idadi hiyo ndogo ya maafisa wa utawala imeathiri shughuli za serikali na kudhoofisha utoaji wa huduma kwa wakazi.

Adhe alisema kuwa kupitia mikutano ya ushirikishwaji wa umma, wakazi walipendekeza kuanzishwa kwa Tarafa ya Telesgaye, lokesheni ya Elbokoch na Ilollo, pamoja na lekesheni ndogo ya Aibete na Lamadang. Hata hivyo, alisema vitengo hivyo bado havijachapishwa rasmi kwenye Gazeti la Serikali wala kuanza kufanya kazi.

Mbunge huyo aliitaka serikali kuharakisha uanzishaji na uendeshaji wa vitengo hivyo vya utawala, akisema hatua hiyo itaongeza uwepo wa serikali, kuimarisha usalama, kuboresha upatikanaji wa huduma za umma na kuimarisha utawala katika eneo hilo la mbali.

Aidha, Adhe alisisitiza kuwa ataendelea kutetea maendeleo yenye usawa katika eneo bunge la North Horr, akisema hakuna jamii inayopaswa kuachwa nyuma katika kupata huduma za serikali.

Radio Jangwani 106.3FM is a community radio station situated in Marsabit County broadcasting from Marsabit town. It is the brain child of the bishop of catholic diocese of Marsabit, Rt. Rev. Peter Kihara. It is established with the objective of reaching the people Marsabit diocese and Marsabit County for evangelization, Education, entertaining and disseminating information to the masses.

1 comment

comments user
Nicholas nyangura

My name is Nicholas Nyangura Hille from Illeret Sub-County.
I would like to take this opportunity to thank Almighty God for the gifts of life and peace. I am sincerely grateful to Almighty God for blessing us with a strong and dedicated Member of Parliament, Hon. Wario Guyo, for his care and commitment to the people of Illeret.
He has represented us well in Parliament and has been a leading ambassador for peace. Through his efforts, he has helped bring together the Gabra and Daasanach communities, ensuring harmony and peaceful coexistence. For nearly four years, our communities have experienced peace without conflict, which is a great achievement.
We appreciate his leadership, dedication, and commitment to the development and unity of our people.
Nicholas Nyangura HilleIlleret Sub-County

Post Comment