Jamaa ashtakiwa kwa tuhuma za kumdunga mwezake kisu.
Jamaa mmoja amefikishwa mahakamani Marsabit kwa tuhuma za kumtishia kumdunga kisu mwenzake baada ya tofauti zao. Kulingana na hati ya mashtaka Mshukiwa Abadallah Guracha, mnamo tariki 15 mwezi huu wa Juni katika lokesheni ya Nagayo Marsabit ya Kati alimtishia kumuangamiza Guyatu Galgallo kwa kumdunga kisu.
Kesi hiyo imewasilishwa mbele ya hakimu mkuu mkazi wa mahakama ya Marsabit Edward Oboge. Mshukiwa ameachiliwa kwa bondi ya shilingi 10,000 pesa taslimu au mdhamini wa shilingi 15,000.
Kesi hiyo itatajwa tena tariki 29 mwezi huu wa Juni.
Wakati uo huo mshukiwa mwingine, Guyo Galgallo Arero kutoka eneo la Manyatta Makaa lokesheni ya Nagayo Marsabit Central ameachiliwa kwa bondi ya shilingi 300,000 pesa taslimu au mdhamini wa shilingi laki 350,000 baada ya kutuhumiwa kumdunga kisu kwenye shavu la kulia Liban Galgallo almaarufu kama HUSTLER siku ya Jumatano tariki 17 mwezi huu wa Juni baada ya kutofautiana. Kesi hii inatarajiwa kutajwa tena tariki 29 mwezi huu wa Juni



Post Comment