Loading Now

Highlights

Marsabit yaenzi miaka 20 tangu ajali ya ndege, wakazi wahimizwa kudumisha amani

Na Nyabande Orwa

Huku ikitimia miaka 20 tangu ajali ya ndege iliyoua watu 14 wakiwemo wabunge sita, maafisa wa serikali na viongozi wa kidini, washikadau wa usalama katika kaunti ya Marsabit wametoa maoni yao kuhusu hali ya usalama katika eneo hili.

Wakizungumza na kituo hiki kwa njia ya simu, viongozi wa kidini na maafisa wa kamati ya usalama wamesema ni muhimu kwa wakazi kuendelea kudumisha amani kama njia ya kuwaenzi waliopoteza maisha yao walipokuwa wakija Marsabit kuhubiri amani. Naibu mwenyekiti wa kamati ya usalama na balozi wa amani, Adan Chukulisa, amesema idadi ya waliofariki kutokana na vita vya kijamii miaka ya nyuma ilikuwa kubwa na haipaswi kujirudia. Amewahimiza wananchi kuchagua viongozi wanaopenda amani katika uchaguzi ujao.

Wakati huo huo, mwenyekiti NCCK  tawi la Marsabit, Saido Diba, amesema kaunti hii imepiga hatua katika kuimarisha amani, akiwataka wanasiasa kuepuka siasa za chuki na badala yake kuunganisha wananchi. Kwa upande wake, mwakilishi wa wanawake, Naomi Wako Jilo, amesema wakazi wanapaswa kuendeleza umoja na amani wanapowakumbuka waliopoteza maisha yao, kwa  harakati za kutafuta Amani ya Marasbit.

Post Comment