Highlights

Zoezi la usajili wa vyeti vya kuzaliwa na vifo laendelea Marsabit

Na Caroline Waforo

Idara ya usajili wa vyeti vya kuzaliwa na vifo inaendesha zoezi maalum la kutoa huduma hizo mashinani katika kaunti ya Marsabit.

Zoezi hilo lililoanza rasmi siku ya Jumatatu linatarajiwa kuendelea hadi tarehe 17 mwezi huu wa Aprili kote jimboni.

Akizungumza na Shajara, Mratibu wa idara hiyo ya usajili wa vyeti vya kuzaliwa na vifo tawi la Marsabit Peter Chetambe, amewahimiza wakaazi kuhakikisha watoto wao wanasajiliwa na kupata vyeti vya kuzaliwa ili kuwawezesha kufaidika na huduma mbalimbali za serikali.

Aidha Chetambe ameweka wazi kuwa idara hiyo inalenga kusajili angalau vyeti vya kuzaliwa 20,000 katika kipindi cha zoezi hilo.

Zoezi hili linaendeshwa sambamba na zoezi la usajili wa vitambulisho vya kitaifa.

Radio Jangwani 106.3FM is a community radio station situated in Marsabit County broadcasting from Marsabit town. It is the brain child of the bishop of catholic diocese of Marsabit, Rt. Rev. Peter Kihara. It is established with the objective of reaching the people Marsabit diocese and Marsabit County for evangelization, Education, entertaining and disseminating information to the masses.

Post Comment