Highlights

Marsabit yaandikisha asilimia 50 tu ya vitambulisho awamu ya kwanza

Na Nyabande Orwa

Kaunti ya Marsabit imefanikiwa kuandikisha asilimia 50 ya watu waliolengwa kupata vitambulisho katika awamu ya kwanza iliyokamilika wiki jana.

Kwa mujibu wa mkuu wa idara ya usajili wa vitambulisho kaunti ya Marsabit, Isaac Kibet, ni watu elfu kumi na tano pekee waliojitokeza kujiandikisha, sawa na nusu ya waliotarajiwa.

Akizungumza na kituo hiki, Kibet amesema kuwa wakazi wengi wa maeneo ya mashinani walikuwa wamehama na mifugo yao, hali iliyofanya zoezi hilo kuwa ngumu licha ya maafisa kuwafuata karibu.

Katika zoezi hilo, kaunti ndogo ya Mopyale iliongoza kwa idadi ya waliojiandikisha ikiwa na watu elfu tano, ikifuatiwa na eneo bunge la Saku lenye takriban watu elfu tatu. Maeneo mengine yalirekodi idadi ndogo zaidi ya waliojitokeza.

Kibet amesema kuwa itachukua takriban siku kumi kwa waliojiandikisha kupata vitambulisho vyao, huku baadhi ya waliokamilisha usajili tayari wakitarajiwa kuvipokea kufikia Ijumaa ya wiki hii.

Amewahimiza wakazi kujitokeza kwa wingi katika awamu ya pili ya zoezi hilo itakayoanza hivi karibuni.

Radio Jangwani 106.3FM is a community radio station situated in Marsabit County broadcasting from Marsabit town. It is the brain child of the bishop of catholic diocese of Marsabit, Rt. Rev. Peter Kihara. It is established with the objective of reaching the people Marsabit diocese and Marsabit County for evangelization, Education, entertaining and disseminating information to the masses.

Post Comment