Highlights

KUPPET yatishia mgomo kuhusu bima ya SHA

Na JB Nateleng

Muungano wa walimu wa shule za upili na vyuo vya kiufundi nchini, KUPPET, umetishia kuitisha mgomo iwapo huduma za bima ya afya ya jamii, SHA, hazitaboreshwa kwa walimu.

Viongozi wa KUPPET kutoka matawi mbalimbali wanasema walimu wanapata shida kupata matibabu kupitia bima hiyo, hasa wale wanaougua saratani, licha ya huduma hizo kuahidiwa.

Katibu Mkuu wa KUPPET tawi la Marsabit, Sarr Galgallo, amesema amepokea malalamishi mengi kutoka kwa walimu kuhusu changamoto wanazokutana nazo wanapotumia SHA.

Akizungumza na kituo hiki kwa njia ya simu, Sarr ameonya kuwa serikali kupitia Wizara ya afya ikichelewa kuchukua hatua, walimu wanaweza kuanza mgomo wakati shule zitakapofunguliwa muhula wa pili wiki ijayo.

Radio Jangwani 106.3FM is a community radio station situated in Marsabit County broadcasting from Marsabit town. It is the brain child of the bishop of catholic diocese of Marsabit, Rt. Rev. Peter Kihara. It is established with the objective of reaching the people Marsabit diocese and Marsabit County for evangelization, Education, entertaining and disseminating information to the masses.

Post Comment