Maonyesho ya sayansi na teknolojia yafanyika katika Shule ya Don bosco Marsabit
Na Sabalua Moses
Maonyesho ya kisayansi na teknolojia yameanza rasmi hii leo kwa siku tatu katika taasisi ya elimu ya Don Bosco ikijumuisha washikadau mbali mbali katika kaunti ya Marsabit .
Akizungumza katika maonyesho hayo mkurugenzi mkuu katika taasisi ya elimu ya Don bosco Fr Sunil Orathel amesema maonyesho hayo yatasaidia pakubwa katika mtaala wa CBE na kuhakikisha wanafunzi wanapata ujuzi wa kisayansi na teknolojia ya kisasa.
Vile vile padre Sunil amesema kupitia kwa taasisi za elimu za kiufundi vijana wanapata mafunzo yatakayo waendeleza kimaisha.
Kwa upande wake naibu mkurugenzi wa Don Bosco Samuel Mutiga amesema madhumuni ya maoonyesho hayo ni kuhakishisha kuwa ujuzi wa wanafunzi unatunzwa na kuelekezwa kwa njia itakayo wasaidia kimaisha.
Naye David Malimo ambaye ni mwanafunzi katika chuo hicho anasema maonyesho hayo yatasaidia wanafunzi kupata ujuzi na maarifa katika mtaala wa CBE.



Post Comment