Highlights

Jamii yahimizwa kuwakumbatia manusura wa saratani

Na JB Nateleng

Jamii ya Marsabit imetakiwa kuwakubali na kuwakumbatia manusura wa ugonjwa wa saratani ili kuwasaidia kurejea katika maisha ya kawaida bila ubaguzi wala unyanyapaa.

Wito huo umetolewa na mtaalamu wa saratani katika hospitali ya rufaa na mafunzo ya Marsabit, Joyce Mukoro, ambaye amesema manusura wa ugonjwa huo hukumbana na changamoto mbalimbali za kimwili na kijamii zinazoweza kubadili mwonekano na mtindo wao wa maisha.

Akizungumza na shajara ya Radio Jangwani ofisini mwake, Mukoro amesema baadhi ya matibabu ya saratani yanaweza kuathiri uwezo wa uzazi wa mgonjwa katika siku zijazo akisisitiza umuhimu wa familia na jamii kuwapa manusura hao upendo, ushirikiano na msaada wa kisaikolojia ili kuwasaidia kukabiliana na changamoto hizo.

Mukoro pia amesema manusura wengi hupitia changamoto za kihisia kutokana na mabadiliko ya mwili na athari nyingine za ugonjwa pamoja na matibabu yake, hali ambayo inaweza kusababisha msongo wa Mawazo.

Post Comment