Highlights

Kaunti ya Marsabit kuendelea kushuhudia vipindi vya jua na ukavu sawa na upepo mkali Loiyangalani.

NA Samuel Kosgei

Utabiri wa hali ya hewa katika kipindi cha siku saba zijazo kuanzia leo tarehe 27 Januari hadi 2 Februari 2026 unaonyesha kuwa Kaunti ya Marsabit itashuhudia hali yajua vipindivya mchana, huku hali ya mawingu kiasi ikitawala nyakati za usiku katika maeneo yote ya kaunti ya Marsabit.

Kwa mujibu wa utabiri huo, mvua haitarajiwi kunyesha katika kaunti nzima ya Marsabit, isipokuwa maeneo machache ya Sagante ambapo matone machache sana ya mvua yanaweza kushuhudiwa

Aidha, upepo wa wastani hadi mdogo kutoka kusini na kusini-mashariki, ukiwa na kasi unatarajiwa katika maeneo kadhaa ya kaunti. Hata hivyo, maeneo mengi ya Loyangalani yanatarajiwa kukumbwa na upepo mkali sana unaozidi kasi 25.

Wananchi wanashauriwa kuchukua tahadhari, hasa wakazi wa maeneo yanayotarajiwa kukumbwa na upepo mkali.

Radio Jangwani 106.3FM is a community radio station situated in Marsabit County broadcasting from Marsabit town. It is the brain child of the bishop of catholic diocese of Marsabit, Rt. Rev. Peter Kihara. It is established with the objective of reaching the people Marsabit diocese and Marsabit County for evangelization, Education, entertaining and disseminating information to the masses.

Post Comment