Diocese of Marsabit

Idara ya Polisi Mjini Marsabit Yaweka Mikakati ya Kukomesha Uhalifu na Wizi za Hivi Karibuni

PICHA: KWA HISANI

Na Samuel Kosgei

Idara ya polisi mjini Marsabit imesema kuwa imeweka mikakati mwafaka ya kukomesha uhalifu na wizi ambao umeonekana kuongezeka mjini Marsabit siku za hivi karibuni.

Afisa mkuu wa kituo cha polisi cha Marsabit Edward Mabonga ameambia shajara kuwa tayari polisi wana habari kuhusu malalamishi hayo ya umma na hivyo tayari polisi wataimarisha doria usiku na mchana ili kukomesha hulka hiyo ya wiizi na uhalifu.

Kauli yake OCS Mabonga inajiri siku chache baada ya wezi wenye silaha kujaribu kuibia duka moja eneo la Shauri Yako viungani mwa mji wa Marsabit wikendi iliyopita.

Maeneo ambayo yametajwa kuongezeka kwa visa vya uhalifu na wizi viungani mwa mji wa Marsabit, ni pamoja  Karantina, Kiwanja Ndege, Majengo na Shauri Yako.

Subscribe to eNewsletter