MILA NA TAMADUNI ZATAJWA KUWA KIKWAZO KWA WANAWAKE KUFANYA MAZOEZI YA MWILI MARSABIT.
November 20, 2024
DCC wa eneo la Marsabit North (Maikona) Pius Njeru amewataka wazazi katika kaunti ya Marsabit kuhakikisha kwamba wanawapeleka watoto shuleni bila kuwabagua.
Akizungumza katika eneo la Kalacha wakati wa hafla ya wazee wa jamii ya Gabra kupiga marufuku tamaduni ya kuwaoza wasichana waliochini ya umri wa miaka 18, DCC Njeru amesema kwamba jamii imeangazia sana mtoto msichana na kumsahau mtoto mvulana ambapo wengi wao wamekosa haki ya elimu kwani wako malishoni.
Aidha DCC Njeru amewataka wazee wa YAA kuunga mkono kikamilifu marufuku ya kuwaoza watoto wachanga ili ipate mafanikio.
Kuhusiana na maswala ya mitihani, DCC Njeru amesema kuwa idara ya usalama imejiandaa kuhakikisha kwamba watahiniwa wote wanakalia mitihani ya kitaifa itayaoanza tarehe 22 mwezi huu.
Kadhalika DCC Njeru ameweka wazi kuwa kuanzia leo jumatatu serekali itawapiga msasa wale watakaojinga na maafisa wa akiba NPR ili kuboresha ulasama katika eneo pana la Marsabit North.