Serikali ya kaunti ya Marsabit yaondolea wazazi wasiwasi kuhusu hatima ya ufadhili wa elimu.
January 21, 2025
Serikali ya kaunti ya Marsabit imesema kuwa itaendeleza zoezi la kuhesabu wafanyakazi wote wa kaunti kabla yam waka kukamilika ili kuendamana na malengo ya serikali sawa na kuimarisha huduma.
Naibu katibu wa kaunti na pia naibu mkuu wa wafanyakazi Doti Tari amesema kuwa lengo kuu la zoezi hilo ni kuimarisha huduma na shughuli za kiserikali.
Zoezi hilo la kuanza kuhesabu wafanyakazi wa serikali ya kaunti ilifanyika wiki jana katika eneobunge la Saku huku shughuli hiyo ikitarajiwa pia kufanyika katika maeneobunge mengine kabla ya mwaka kutamatika. Hilo anasema imetatizwa kwa sasa na ukosefu wa fedha kufadhili shughuli hiyo.
Doti ameongeza kuwa lengo lingine la kufanya hesabu hiyo ni ili kujua idadi kamili ya wafanyakazi wanaofika kazini na kuhakikisha kuwa kazi ya mtu inaendana na ujuzi na taaluma aliyosomea.
Anasema kupitia hilo watazuia kuchanganya taaluma aliyosomea mtu na kazi anayofanya kwa sasa.
Orodha mpya ya waajiriwa itakapotolewa anasema itasaidia kuyaondoa majina ya watu waliofariki au hata kustaafu kati ya nyingine.
Mnamo tarehe 7 November mwaka huu ofisi ya mkuu wa wafanyakazi na bodi ya kuajiriwa wafanyakazi wa umma iliendesha zoezi hilo katika kaunti ndogo ya Saku.