Vijana wazidi kutiwa shime kupigania haki zao nchini.
January 21, 2025
Mkurugenzi wa elimu kaunti ya Marsabit Peter Magiri ameshutumu wazazi na walimu ambao wanazidi kulipa pesa ili watoto wao wadanganye kwenye mitihani ya kitaifa ya darasa la sita KPSEA.
Magiri akizungumza na walimu kwenye mkutano wao wa kufunga mwaka ulioandaliwa mjini Marsabit amesema ni swala la kushangaza kuona bado walimu wanazidi kutoa pesa kununua mitihani ilhali hakuna mashindano kati ya wanafunzi kama ilivyokuwa miaka ya hapo nyuma wakati wa KCPE.
Ameonya wote wanaendeleza hulka ya kuibia wanafunzi akisema kuwa hilo limepitwa na wakati kwa hakuna mashindano tena kati ya shule moja hadi nyingine.