Vijana wazidi kutiwa shime kupigania haki zao nchini.
January 21, 2025
Wito umetolewa kwa wazazi kuwapeleka wanawao hospitalini iwapo wataripoti visa vyovyote vya kuumwa na macho. Haya yamekaririwa na mtaalam wa macho katika kliniki ya Macho, katika hospitali ya rufaa ya Marsabit Amina Duba.
Akizungumza na idhaa hii afisini mwake, Amina amesema kuwa kuna magonjwa ya macho ambayo yanaweza yakatibika iwapo yatagunduliwa mapema na kupewa tiba sahihi.
Amina amesema kuwa kuna magonjwa ya macho ambayo mtoto anazaliwa nayo na yanaweza yakatibiwa iwapo mama atajifungulia hospitalini.
Hata hivo Amina amewashauri wazazi kuacha kununua dawa kutoka dukani ili kutibu magonjwa ya macho na badala yake wawapeleke wanawao kwa mtaalam wa Macho ili waweze kupata tiba kamili.
Mtaalam huyu amesema kuwa serekali bado inaendelea kutoa hamasa kwa watoto shuleni na pia wazazi manyumbani kuhusu umuhimu wa kutunza macho ili kujikinga dhidi ya magonjwa ya macho.
Wito huu unajiri wakati ambapo dunia inajiandaa kusherehekea siku ya macho duniani, tarehe 10 oktoba 2024. Katika kaunti ya Marsabit sherehe hiyo itaandaliwa katika eneo la Log logo eneo bunge la Laisamis.