County Updates, Diocese of Marsabit, Editorial, Local Bulletins, National News

WITO WATOLEWA KWA JAMII YA MARSABIT KUWALINDA WATOTO HASWA WAKATI WA LIKIZO NDEFU YA MWEZI DISEMBA MWAKA HUU.

Na Isaac Waihenya,

Wito umetolewa kwa wananchi Marsabit kuhakikisha kwamba wanawalinda watoto haswa wakati wa likizo ndefu ya mwezi Disemba mwaka huu.

Kwa mujibu wa afisa wa watoto katika kaunti ya Marsabit Mukanzi Leakey ni kuwa visa vya dhulma za watoto vimepungua katika kaunti ndogo za Moyale,Saku na North Horr huku kaunti ndogo ya Laisamis ikisalia kuwa kaunti ndogo inayoripoti idadi kubwa ya visa hivyo.

Akizungumza na Radio Jangwani ofisini mwake Leakeay ametaja kwamba idadi ya visa vya wazazi kuwatelekeza watoto vimeongezeka katika kaunti ndogo hizo.

Aidha Leakey amewataka wazazi kukumbatia mbiinu za kusuluhisha mizozo mashinani ili kuhakikisha kwamba watoto hawaadhiriki zaidi kutokana na mizozo ya kiboma.

Kadhalika afisa huyo wa watoto jimboni amekariri kuwa idara hiyo imeweka mikakati kabambe ambayo imepelekea visa vya wasichana kuvukishwa mipaka na kukeketwa na kisha kurejeshwa kupungua kwa asilimia kubwa.

Subscribe to eNewsletter