County Updates, Diocese of Marsabit, Editorial, Local Bulletins, National News

WAZEE WA JAMII YA GABRA (YAA) WAPIGA MARUFUKU TAMADUNI YA KUWAOZA WASICHANA WALIOCHINI YA MIAKA 18.

Sasa ni afueni kwa wasichana kutoka jamii ya Gabra katika kaunti ya Marsabit baada ya wa wazee wa jamii hiyo maarufu YAA kupiga marufuku tamaduni ya kuwaoza wasichana waliochini ya miaka 18.

Hafla hiyo iliyofanyika katika eneo la kitamaduni, katika kijiji cha Kalacha na kufadhiliwa na shirika la kutetea haki za binadamu la IREMO iliwaleta pamoja viongozi wa kijamii,wale wa serekali na mashirika mbalimbali ambapo kwa pamoja makukubaliano ya kukomesha mila hiyo ambayo imekuwa ikihujumu elimu yaliafikiwa.

Akizungumza katika hafla hiyo mkurugenzi mkuu wa shirika la IREMO, Darare Gonche ambaye pia ni MCA mteule ametaja kuwa ni jambo la kufurahia kuona kuwa safari hiyo iliyoanza miaka saba iliyopita imepata ufanisi.

Aidha mkurugenzi wa shirika la IREMO Lokho Abduba amepongeza hatua hiyo huku akifichua kwamba jamii zingine zimeweka wazi nia ya kusitasitisha mila hii kabla ya mwaka huu wa 2024 kutamatika.

Kwa upande wake mkurugenzi mkuu wa shirika la kutetea haki za binadamu katika kaunti ya Marsabit MWADO, Bi. Nuria Golo ambaye pia alihudhuria hafla hiyo amewataka wazee kuwa mabalozi wema ili kuhakikisha kwamba ujumbe kuhusiana na marufuku ya ndoa za mapema unafika mashinani.

Baadhi ya wanajamii wakiongozwaa na Sarah Peters wameitaja hatua hiyo kama itakayopiga jeki elimu ya wasichana hapa jimboni Marsabit.

Subscribe to eNewsletter