County Updates, Diocese of Marsabit, Editorial, Local Bulletins, National News

WAZAZI WATAKIWA KUWALINDA WANAO HASWA WAKATI WA LIKIZO NDEFU YA MWEZI DISEMBA ILI KUWAEPUSHA NA DHULMA ZA KIJINSI

Na Isaac Waihenya & Abdiaziz Abdi & Kame Wario,

Wazazi wametakiwa kuwalinda wanao haswa wakati wa likizo ndefu ya mwezi disemba ili kuwaepusha na dhulma zozote dhidi yao.

Kwa mujibu wa afisa anayesimamia maswala ya jamii katika shirika lisilokuwa la kiserekali la SIF hapa jimboni Marsabit Halima Hirbo ni kuwa ni jukumu la wazazi kuhakikisha kwamba wanao wako salama msimu wa likizo.

Akizungumza na Radio Jangwani baada ya kuandaa mkao wa kutoa mafunzo kwa wazazi na walezi wa watoto wanaonufaika na mradi wa elimu unaofadhiliwa na shirika hilo,Halima amewataka wazazi kuwajukumisha wanao katika majukumu ya kinyumbani ili kuwaepusha na maswala yanayoweza kuwadhuru kama vile utumizi wa miharati na dawa za kulevya.

Aidha Halima amewaonya wazazi dhidi ya kuwaoza na kuwakeketa wasichana katika msimu huo wa likizo akisema kuwa watakaopatikana wakiendeleza uovu huo watachukuliwa hatua kali za kisheria.

Aidha wazazi waliopokea mafunzo hayo wamekariri kuwa watahakikisha kwamba wanatilia maanani mafunzo kuhusiana na jinsi ya kuwatunza wanao huku wakilishukuru shirika la SIF kwa kuhakikisha kwamba wanao wanapata haki ya elimu kama watoto wengine hapa nchini.

Subscribe to eNewsletter