Vijana wazidi kutiwa shime kupigania haki zao nchini.
January 21, 2025
Wazazi washauriwa kuasi miendendo ambayo inasababisha wao kutelekeza majukumu ya kuwalea wanawao.
Kwa mujibu wa mchungaji wa kanisa la PEFA hapa jimboni Marsabit Daudi Wako ni kuwa wazazi wanafaa kuhakikisha kuwa wanawao wanapokea malezi bora wakati huu wa likizo.
Akizungumza na idhaa hii kwa njia ya kipekee,Wako ameelezea kuwa ni sharti wazazi wawe wakisuluhisha migogoro yao mbali na watoto ili kuwaepusha na matatizo afya ya kiakili ambayo itawapelekea wao kukosa amani katika maisha yao.
Wako amesema kuwa ni jukumu la wazazi kuelekeza watoto kwa njia inayofaa kwa ajili ya vizazi vijavyo akisema kuwa hilo litasaidia katika kujenga jamii bora.
Kadhalika Wako amewarai wazazi kuhakikisha kuwa watoto wanahurudhuria mafunzo ya dini ili kujifunza na kujiboresha kiimani wakati huu wa likizo ya mwezi Disemba.