Serikali ya kaunti ya Marsabit yaondolea wazazi wasiwasi kuhusu hatima ya ufadhili wa elimu.
January 21, 2025
Wazazi katika kaunti ya Marsabit wametakiwa kuwa wangalifu kipindi hichi likizo ili kuhakikisha kwamba wanao hawajiingizi katika utumizi wa mihadarati.
Kwa mujibu wa mwalimu Sarah Wanyeki ni kuwa ni jukumu la wazazi kujua waliko wanao kipindi cha likizo ili wasije wakajihisisha na maovu.
Akizungumza na Shajara ya Radio Jangwani kwa njia ya kipekee, Bi. Sarah amewataka wazazi kuwahusisha watoto na maswala ya dini ili wadipotoke kimaadili.
Bi. Sarah ameweka wazi kuwa ni kinyume cha Sheria kuwakeketa na hata kuwaoza watoto huku akiwataka wazazi kuhakikisha kwamba wanao hawapitii dhulma hiyo.
Aidha Bi. Sarah amekariri hoja ya wazazi kuwa waangalifu na kufuatilia wanachofanya wanao kwenye mitandao ya kijamii ili kuwaepusha na maadili mabaya. Na mafunzo yasiyofaa