Vijana wazidi kutiwa shime kupigania haki zao nchini.
January 21, 2025
Wazazi katika kaunti ya Marsabit wametakiwa kutowaficha watoto wanaoishi na ulemavu na badala yake kuwapeleka shule ili wapate elimu.
Kwa mujibu wa mshiriki wa baraza la watu wanaoishi na ulemavu (NCPWD) kaunti ya Marsabit Ahmed Abdi,ni kuwa watoto wanaoishi na ulemavu wanafaa kupewa haki sawa na wale wengine.
Akizungumza na Shajara Ya Radio Jangwani ofisini mwake Abdi amelitaja swala na kuwaficha watoto wanaoishi na ulemavu kama kuhujumu haki zao za kimsingi.
Aidha Abdi amewataka wananchi wa Marsabit walio na ulemavu au wanaoishi na watu waliona ulemavu kuchukua fomu za kujisaji katika ofisi hiyo ili kuhakikisha kwamba wanapata misaada na huduma zinazotoka katika serekali kuu.
Hata hivyo Abdi amekanusha madai kuwa ofisi yake imekuwa ikiwazuia wanagenzi maarufu Interns kupata nafasi huku akiwataka waliona malalamishi kuyawasilisha kwake.