Vijana wazidi kutiwa shime kupigania haki zao nchini.
January 21, 2025
Wazazi katika kaunti ya Marsabit wameshauriwa kutolegeza kamba kwa wanao haswa msimu huu wa likizo ili kuzuia wasichana kupata mimba za utotoni.
Kwa mujibu wa afisa wa watoto katika kaunti ya Marsabit, Abudho Roba ni kuwa baadhi ya mimba za mapema kwa wasichana zinaweza epukika iwapo wazazi watatekeleza majukumu yao ya ulezi ipasavyo.
Akizungumza na Shajara ya Radio Jangwani ofisini mwake Abudho amesema kuwa vijana wengi wanajihusisha katika ngono za mapema jambo linalochangia pia uwepo wa mimba za utotoni.
Pia afisa huyo wa watoto amewarai wazazi kuwa waangalifu na jinsi watoto wao wanavyotumia simu kwani wengi wanapoteza muda wao kwa simu kuangalia vitu ambavyo haviwasaidii.
Aidha ametoa wito kwa wazazi kuchukua udhibiti na kujua mahali wanapoenda wanao na kuwashauri huku akiwataka kuwawajibisha katika majukumu mandogo mandogo ya kinyumbani.