Vijana wazidi kutiwa shime kupigania haki zao nchini.
January 21, 2025
Wazazi katika kaunti ya Marsabit wahimizwa kuwajibika kwa kuchunga wanao katika kipindi cha likizo ndefu ya mwezi Disemba.
Huku wanafunzi wakitarajiwa kuelekea likizo ndefu ya mwezi disemba, wazazi katika kaunti ya Marsabit wamehimizwa kuwajibika kwa kuchunga wanao kipindi hicho cha likizo.
Ushauri huo umetolewa naye mkurugenzi mkuu wa shirika la kutetea haki za binadamu la Inua Dada Mashinani katika kaunti ya Marsabit Bi. Jillo Fugicha.
Akizungumza na Shajara ya Radio Jangwani ofisini mwake, Fugicha amesema kuwa ni jukumu la wazazi kujua mienendo ya wanao na wale wanaotengamana nao ili kuwazuia kupotoshwa kimaadili.
Aidha Fugicha amewaonya wazazi dhidi ya kuwakeketa wala kuwaoza wasichana wakati wa likizo akikariri kuwa watakaopatikana wakiendeleza uovu huo watachukuliwa hatua kali za kisheria.
Kadhalika amewataka wazazi kuwajukumisha watoto wakati huu wa likizo na wala sio kuwapa kazi nzito kuliko umri wao.
Hata hivyo mtetezi huyu wa haki za binandamu jimboni Marsabit amewapongeza wazee wa jamii ya Gabra maarufu YAA kwa kupiga marufuku zoezi la kuwaoza wasichana waliochini ya umri wa miaka 18 huku akizitaka jamii zingine jimboni kuiga mfano huo.