MILA NA TAMADUNI ZATAJWA KUWA KIKWAZO KWA WANAWAKE KUFANYA MAZOEZI YA MWILI MARSABIT.
November 20, 2024
Na Naima Abdullahi & JB Nateleng,
Dawa za kienyeji huenda zikawa za manufaa iwapo madaktari wa kienyeji watakaguliwa na kutathminiwa na idara husika kwa manufaa ya wanaoitumia.
Haya ni kwa mujibu wa daktari Adan Abdullahi ambaye ni mtaalam wa dawa katika hospitali ya rufaa ya Marsabit.
Akizungumza na idhaa hii kwa njia ya kipekee, daktari Abdullahi ameelezea kuwa idadi kubwa ya watu jimboni imeshabikia matumizi ya dawa za kienyeji kwa sababu zinapatikana kwa urahisi na si ghali hivyo kutoa wito kwa serekali kuu na serekali ya kaunti pamoja na washikadau wa afya kubuni sheria ambayo itaboresha usalama wakati wa matumizi ya dawa hizi.
Kulingana naye, dawa za kienyeji ni afueni kwa sababu zinatoka kwa mimea ambayo kwa kiwango kikubwa inapatikana katika misitu na pia manyumbani.
Aidha daktari Abdullahi ameelezea kuwa iwapo serekali haitadhibiti matumizi ya dawa za kienyeji basi huenda watu wengi wakaathirika kwa sababu dawa hizi hazina kipimo, hata pia wanaozitumia hawaelewi namna zinavyofaa kutumika.