Wito umetowa kwa wanaume kuweza kujitokeza na kuripoti visa vyovyote vya dhuluma wanazopitia ili waweze kusaidika.
Kwa mujibu imamu wa msikiti wa Jamia hapa mjini Marsabit Sheikh Mohamed Noor, Wanaume wanapitia changamoto si haba ambayo japo wengi wao huamua kunyamaza jambo ambalo linawafanya kuathirika zaidi kimawazo.
Akizungumza na idhaa hii kwa njia ya kipepee, Sheikh Noor ameitaka jamii kuweza kuwajali na kuangazia changamoto wanazopitia wanaume akisema kuwa hili litawasaidia kufunguka.
Hata hivo Sheikh Noor amewashauri wanaume kusaidia na wake wao katika kuwalea watoto msimu huu wa likizo ambapo Watoto wapo nyumbani kwa miezi miwili.
Kadhalika Sheikh Noor ametoa wito kwa serekali pamoja na mashirika yasiyokuwa ya kiserekali kutoa hamasa kwa wanaume pamoja na Watoto wa kiume kuweza kujitokeza na kuripoti dhulma wanazopitia badala ya kunyamaza.