Vijana wazidi kutiwa shime kupigania haki zao nchini.
January 21, 2025
Baadhi ya wakaazi wa Marsabit wamepewa mafunzo kuhusu namna ya kutumia meko ya kisasa kupikia chakula ikiwa ni lengo mojawapo ya taifa la Kenya kufikia asilimia 100 ifikapo 2028 katika kupika na meko yenye kukabili hewa chafu.
Akizungumza na idhaa hii kwa njia ya kipekee afisini mwake mkurugenzi mkuu katika idara ya Kawi Joseph Agola amewarai wakaazi wa Marsabit wazingatie njia mwafaka ili kufikia lengo hilo.
Baadhi ya majukumu ambayo Agola amesema wameweka mikakati ni kuyafunza makundi ya akinamama njia ya kutengeneza jiko safi au jikokoa, makaa ya kuni, na kusambaza mbegu ya mti katika shule mbalimbali ili kutunza mazingira.
Aidha Agola ametaja kuwa wamekumbwa na changamoto kama vile kukosa njia mwafaka ya kuuza meko ambazo vikundi vya akina mama wameweza kutengeneza kutokana na ukosefu wa usafiri mwafaka kati ya nyingine.