Vijana wazidi kutiwa shime kupigania haki zao nchini.
January 21, 2025
Huku ulimwengu ukiadhimisha siku ya mazingira hii leo wananchi kaunti ya Marsabit wametakiwa kuasi kasumba ya kukata miti ili kupambana na mabadiliko ya tabia nchi.
Akizungumza kwenye warsha ya kusherehekea siku ya Mazingira hapa Marsabit mkurugenzi wa Mazingira katika jimbo la Marsabit Janet Ahatho amewataka wakazi wa Marsabit kuishabikia zoezi la Upanzi wa miti ili kupambana na mabadiliko ya tabianchi.
Amesema kuwa ili kufikia lengo la kitaifa la upanzi wa mti jimboni, ni sharti kila mmoja achukue jukumu la kupanda angalau miche 30 kila msimu wa mvua.
Mkurugenzi huyu amedokeza kuwa ni jukumu la kila mmoja kupanda miti kwa ajili ya kutunza mazingira na pia uhai wa kila mmoja ili kuepuka mafuriko pamoja na ukame ambayo ilikuwa imekumba kaunti ya Marsabit miaka zilizopita.
Junet ameitaka serekali kuweza kudhibiti mpaka wa Kenya na kaunti jirani ya Ethiopia ambayo haijapiga marufuku matumizi ya karatasi za plastiki.
Kauli yake imeweza kuungwa mkono na mwenyekiti wa Marsabit Walk Movement Konse Kura akisema kuwa jamii inafaa kukumbatia upanzi wa mti ili kuepusha madhara ambayo yanatokana na mabadiliko ya Tabianchi.