Vijana wazidi kutiwa shime kupigania haki zao nchini.
January 21, 2025
Na Naima Abdullahi & Kame Wario,
Huku ulimwengu ukiadhimisha siku ya wazee duniani hapo jana,jamii ya Marsabit imetakiwa kuwatunza wazee ili kuwaepusha na madhara.
Kwa mujibu wa afisa wa huduma za jamii katika kaunti ya Marsabit Habiba Ailo Adan ni kuwa jamii inafaa kuwatunza wazee na kuasi kasumba ya kuwatelekeza.
Akizungmza na Shajara ya Radio Jangwani Ailo amewarai wananchi wa Marsabit kujumuisha wazee kwa miradi ya jamii ili wasikue na upweke.
Aidha baadhi ya wazee waliozungumza na Shajara ya Radio Jangwani wamelalamika kwamba hawajanufaika na pesa za wazee wakidai kuwa walitengwa wakati wa watu kusajiliwa huku wengine wao wakiishukuru serikali kuu kwa kujali maslaha ya wazee na kuwapa msaada wa pesa ili wajimudu kimaisha.