Serikali ya kaunti ya Marsabit yaondolea wazazi wasiwasi kuhusu hatima ya ufadhili wa elimu.
January 21, 2025
Idara ya elimu kaunti ya Marsabit imeongeza kiwango cha walimu katika shule za msingi,msingi sekondari (JSS) na shule za upili.
Kulingana vyanzo vya habari kutoka tume ya huduma za walimu TSC, vilivyosema na Shajara ya Radio Jangwani kwa njia ya kipekee ni kwa takriban walimu 426 waliajiriwa kwa mkataba wa kudumu katika kaunti ya Marsabit mapema mwezi huu.
Katika idadi hiyo walimu 289 ni wale wa sekondari msingi JSS, walimu 127 wakiwa na shule za msingi huku walimu 10 wakiwa ni wa shule za upili, zoezi hili likilenga kuziba mianya ya upungufu wa walimu katika kaunti ya Marsabit.
Hata hivyo zoezi la kuwaajiri wanagenzi maarufu Interns linaendelea katika kaunti ndogo zote hapa jimboni Marsabit.
Wanagenzi hao wanatarajiw akuziba pengo la ukosefu wa walimu katika shule za msingi sekondari JSS haswa gredi ya 7,8 na 9.