KITUO CHA KUOKOA WANAOPITIA DHULMA ZA KIJINSIA KUANZISHWA LOGLOGO KAUNTI YA MARSABIT
November 6, 2024
Wakaazi wa Marsabit wamehimizwa kutumia bima ya mifugo ilikuepukana na athari ya janga la ukame ,hii ni kwa mujibu wa afisa wa uhusiano mwema katika idara ya mifugo Asha Galgallo
Akizungumza na idha hii afisini mwake Galgalo amesema kuwa kwa sasa Watu elfu nane wamejisajili tangu bima hiyo kuanza lakini bado wakaazi wengi hawajajisajili ili kufaidi na bima hiyo.
Aidha Galgallo ametaja baadhi ya changamoto zinazowaathiri wafugaji kutojisajili na bima hii ikiwemo elimu duni, maisha ya kuhamahama, na kutolipwa bonasi na kampuni ya bima kwa waliojisajili.
Pia amewarai wakaazi wa jimboni Marsabit wajisajili kwa bima hiyo kwa sababu ni muhimu na inasadia wakati wa ukame na ni kinga wakati wa janga.