Vijana wazidi kutiwa shime kupigania haki zao nchini.
January 21, 2025
Na Isaac Waihenya & Abiaziz Abdi & Kame Wario,
Wakaazi wa Marsabit wametoa hisia zao kuhusiani na kuwepo kwa njama za kumbandua mamlakani naibu wa rais Rigathi Gachagua.
Baadhi ya waliozungumza na Shajara ya Radio Jangwani wametaja kwamba iwapo kuna njama ya kumgo’a mamlakani naibu wa rais Rigathi Gachagua, basi anafaa kuondoka pamoja na Rais Wiliam Ruto kwani wawili hao walichaguliwa kwa tiketi moja.
Wametaja kwamba Rigathi hajafanya kosa lolote kama inavyoashiriwa na baadhi ya viongozi wanaosukumiza ajenda ya kutaka kubanduliwa kwake.
Aidha wengine wao wamehisi kuwa Gachagua anaubeba msalaba wake kutokana na kile wamekitaja kuwa ni kukaidi mkubwa wake Rais Wiliam Ruto na hata kujihusisha na siasa za mapema za mwaka wa 2027.
Hata hivyo baadhi yao wamelaumu ujio wa kinara wa Azimio Raila Odinga serekalini huku wakimtaja kama chanzo cha mzozo kati ya rais na naibu wake.