Vijana wazidi kutiwa shime kupigania haki zao nchini.
January 21, 2025
Baada ya waziri wa usalama Profesa Kithure Kindiki kuapishwa kama naibu wa rais mpya hii leo, wakaazi wa kaunti ya Marsabit wametoa hisia zao kuhusiana na hatua hiyo.
Baadhi ya waliozungumza na shajara ya Radio Jangwani kwa njia ya kipekee, wameonyesha kutoridhishwa na uamuzi uliofanywa na mahakama pamoja na Rais Ruto kwa kumchagua Kithure Kindiki kuwa naibu wa rais mpya.
Hata hivyo wengine wao wamempongeza Professa Kindiki kwa kuchaguliwa kama naibu wa rais na kumtaka Kindiki kushirikiana na Rais Ruto kuwafanyia kazi wananchi.