Vijana wazidi kutiwa shime kupigania haki zao nchini.
January 21, 2025
Wakaazi wa kaunti ya Marsabit wametakiwa kuendelea kutoa ripoti muhimu kuhusiana na visa vya ugaidi na itikadi kali ili kuhakikisha kwamba taifa liko salama.
Kwa mujibu wa afisa wa mipango katika shirika la SND Wako Boru ni kuwa wananchi wanafaa kutoa ripoti zote muhumu kwa maafisa wa usalama ili kuzuia mafunzo ya itikadi kali kuendelea hapa jimboni.
Akizungumza na Shajara Ya Radio Jangwani kwa njia ya kipee,Wako ameyataka mashirika yasiyoyakiserekali jimboni kupiga jeki kamati iliyobuniwa kusaidia katika kupambana na swala hilo hapa jimbini Marsabit ili kuziba miaya yote inayoweza kutumika na wahalifu.
Aidha Wako amewataka waliopewa mafunzo kuhusiana na namna ya kuzuia mafunzo na hata uwepo wa visa vya itikadi kali jimboni Marsabit, kuwa mabalozi wema na kuhakikisha kwamba maarifa waliyoyapa yafikia wananchi vijijini.