Vijana wazidi kutiwa shime kupigania haki zao nchini.
January 21, 2025
Na Talaso Huka,
Wakaazi wa kaunti ya Marsabit wametoa hisia kinzani kuhusiana na mapendekezo ya Senata wa Nandi Samson Cherargei ya kutaka kuongezewa kwa muda wa muhula wa kutalawa kutoka miaka mitano hadi miaka saba.
Baadhi ya waliozungumza na Radio Jangwani wametaja kughadhabishwa na pendekezo hilo huku wakitaja kwamba viongozi wa kisiasa wanafaa kuangazia maslahi ya wananchi na kuzungumzia maendeleo nchini badala ya kuangazia siasa.
Hata hivyo wengine wao wameunga mkono pendekezo hilo na kutaja kwamba kuwa viongozi wanahitaji muda mrefu ili kutumiza ahadi walizotoa kwa wananchi.