Viongozi wa kidini wakemea kisa cha mauaji ya mapacha Dukana, Marsabit
January 24, 2025
Na JB Nateleng & Naima Abdullahi,
Wito umetolewa kwa wakaazi wa kaunti ya Marsabit kukumbatia mfumo wa kilimo Kinachohimili Mabadiliko ya Tabianchi (climate smart) ili kuboresha ukuzaji wa mimea na kuongeza mavuno jimboni.
Akizungumza na idhaa hii kwa njia ya simu, Mkurugenzi katika idara ya Kilimo Patrick Gitu amesema kuwa mfumo huu ni rahisi na unahitaji ujuzi mdogo sana kuufanikisha.
Gitu amesema kwamba mfumo huo utasaidia katika kuboresha usalama wa chakula kwa sababu unatumia vifaa ambavyo vinauwezo wa kukuza na kulinda mimea.
Kulingana na Gitu, serekali ya kaunti ya Marsabit inashirikiana na washikadau mbalimbali kuhakikisha kuwa wakaazi wa Marsabit wanahamasishwa zaidi ili kuukumbatia mfumo huo.
Gitu amesema kuwa japo kuna uhaba wa maji katika kaunti ya Marsabit wakulima kutoka maeneo bunge ya Moyale na Saku wamekumbatia mfumo huo na kuusifia kuwa unasaidia kwa kiwango kikubwa.
Aidha Gitu amesema kuwa mfumo huu ambao ulianzishwa jimboni Marsabist miaka 10 iliyopita bado unaendelea kuboreshwa ili kufikia idadi kubwa ya watu jimboni.