Vijana wazidi kutiwa shime kupigania haki zao nchini.
January 21, 2025
Huku seneti ikizidi kusikiliza kesi dhidi ya kuondolewa kwa naibu rais rigathi Gachagua, baadhi ya wakaazi wa kaunti ya Marsabit wameelezea maoni yao kinzani kuhusu hatma ya Gachagua.
Baadhi wameunga mkono kuondolewa kwake huku wengine wakipinga mpango huo wakidai kuwa Gachagua hana hatia bali anawindwa kisiasa.
Baadhi ya wanaopinga mchakato huo wameonesha Imani kuwa Gachagua ataokolewa na mahamakama.
Wakati uo huo wale wanaounga mchakato huo wa kuondolewa kwa Rigathi Gachagua wamedai kuwa masaibu anayoyapitia ni msiba wa kujitakia kwani amekuwa akitoa matamshi ya kutenganisha taifa.